Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United kumkosa Yoro kwa miezi mitatu

Leny Yoro .png Man United kumkosa Yoro kwa miezi mitatu

Wed, 7 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Manchester United itamkosa beki wake mpya, Leny Yoro kwa muda wa miezi mitatu baada ya mchezaji huyo kufanyiwa upasuaji wa mguu wake wa kushoto.

Yoro (18) alipata maumivu ya enka katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Arsenal, Julai 28 ambayo yalionekana yatamuweka nje kwa muda wa wiki sita hapo awali.

Hata hivyo mambo yamekwenda tofauti na sasa beki huyo aliyesajiliwa katika dirisha hili la majira ya kiangazi kutoka Lille ya Ufaransa, atakosekana kwa muda wa miezi mitatu.

Juzi Jumatatu, Yoro alifanyiwa upasuaji huo na klabu yake imethibitisha kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa miezi mitatu akiuguza majeraha yake.

“Tunatazamia atarejea katika ufiti ndani ya miezi mitatu,” ilifafanua taarifa ya Man United.

Beki huyo mwenyewe amewashukuru mashabiki wa klabu hiyo kwa jumbe za kumtakia heri ambazo wanamtumia.

“Huu sio mwanzo ambao nilihitaji lakini ndio mpira wa miguu. Upasuaji umeenda vizuri, asanteni kwa jumbe zenu za sapoti.

“Sasa ni muda wa uvumilivu na kazi ya ukarabati. Tutaonana muda mchache ujao nikiwa imara,” amesema Yoro.

Yoro alinunuliwa kwa ada ya Pauni 52 milioni kutoka Lille, Julai 18 na hadi sasa ameichezea Man United mechi mbili tu zote zikiwa za rafiki dhidi ya Rangers na Arsenal.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live