Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag amesema wanatarajia kufanya uchunguzi wa ndani kubaini sababu za wachezaji wake kuumia mara kwa mara ikiwa ni siku chache baada ya Lisandro Martinez na Victor Lindelof kupata majeraha.
Walinzi hao wanatarajiwa kuwa nje kwa mwezi mmoja, Martinez akipata majeraha ya kiazi cha mguu, Lindelof akiumia nyama za paja, hivyo kuungana na walinzi wengine Luke Shaw na Tyrell Malacia nao bado ni majeruhi.
Mpaka sasa United ina wachezaji nane majeruhi wa kikosi cha kwanza huku ikicheza jana Aprilli 4, 2024 dhidi ya Chelsea katika #PremierLeague, na kupoteza kwa kufungwa bao 4-3.