Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United inawataka mastraika hawa!

Mbappe Man U Mbappe

Sat, 4 Mar 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Licha ya kiwango bora cha Murcus Rashford kwa sasa, kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson ameendelea kusisitiza kwamba timu hiyo bado inahitaji straika halisi ili kufanya vizuri zaidi staa huyo bado hatoshi.

Suala la straika liliwahi kujadili tangu dirisha lililopita la majira ya baridi na akasajiliwa Wout Weghorst kutoka Burnley  ili kucheza eneo hilo lakini kiwango chake hakionekani kuwaridhisha watu wengi na kuna uwezekano asirejee kwenye kikosi hicho baada ya mkataba wake wa sasa wa mkopo kumalizika.

Lakini je? baada ya staa huyo kuondoka ni wachezaji gani wengine wanaoweza kusajiliwa na Man United ili kucheza kwenye eneo hilo. Hawa hapa mastraika watano wanaoweza kusajiliwa na Man United katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Lautaro Martinez Miongoni mwa wachezaji muhimu sana kwenye kikosi cha Inter Milan na aliisaidia wababe hao kuchukua ubingwa wao wa kwanza baada ya muda mrefu msimu wa 2020/21.

Lautaro  kuna wakati amewahi kuwaniwa na Barcelona lakini dili likafeli. Msimu huu amecheza mechi 34 za michuano yote na amefunga mabao 16 sambamba na asisti saba.

Anatajwa kuwa kwenye orodha ya mastraika wanaoweza kutua kwenye kikosi cha mashetani wekundu ingawa changamoto kubwa ni mkataba wake mrefu unaotarajiwa kumalizika mwaka 2026.

Ingawa taarifa kutoka Italia zinadai kwamba staa huyo huenda akauzwa kwa kiasi kisichozidi Pauni 60 milioni na ilitamani sana kumuuza mwaka jana ili iweze kumsajili Paul Dybala lakini hakukuwa na ofa iliyofikia matakwa yao.

Harry Kane Moja kati ya usajili ambao unafikiriwa sana na mabosi wa Man United ni huu kwa sababu tayari fundi huyu anaifahamu vizuri Ligi Kuu England hivyo kwa namna yoyote hatohitaji muda mrefu sana kuzoea mazingira ya ndani na nje ya uwanja.

Vilevile inaonekana itakuwa rahisi kumsajili kwa sababu mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu ujao, hivyo akigoma kusaini mkataba mpya Spurs italazimika kumuuza katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ili kupata walau kiasi kikubwa cha pesa kwani akikaa hadi dirisha la majira ya baridi atauzwa kwa pesa ndogo zaidi.

Kane ni miongoni mwa wachezaji wasiokuwa na shaka kwenye suala la kufunga akiwa na wastani wa kufunga mabao 20 au zaidi kwa zaidi ya misimu minne sasa.

Victor Osimhen Stori zimekuwa nyingi kuhusiana na fundi huyu. Timu nyingi barani Ulaya zinatamani kuipata huduma yake katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi kutokana na kiwango alichoonyesha kweye michuano mbali mbali akiwa na Napoli kwa msimu huu.

Hata hivyo, kwa timu yoyote itakayokuwa inahitaji huduma yake inaelezwa kwamba itatakiwa itoe kiasi kisichopungua Pauni 90 milioni ama zaidi ya hapo.

Mabosi wa Napoli hivi karibuni walidai kwamba wapo tayari kumuuza Osimhen na Man United ikienda mezani haitokataa ingawa watatakiwa walipe pesa ambayo itakuwa thamani sawa na kiwango cha mchezaji huyo kwa sasa.

Osimhen mwenyewe ameonekana kutamani sana kuondoka lakini amedai wenye uamuzi wa mwisho ni timu kwa sababu ana mkataba hadi mwaka ...

Dusav Vlahovic Inadaiwa kuwa Ten Hag ni shabiki mkubwa wa staa huyu na anatamani kufanya naye kazi kutokana na kiwango chake.

Staa huyu wa kimataifa wa  Serbia msimu huu amefunga mabao tisa kwenye mechi 18 za michuano yote ikiwa ni miongoni mwa misimu mibaya kwake.

Hata hivyo bado kiwango chake kilichomtoa Fiorentina kwenda Juventus kimeendelea kuishi kwenye mawazo ya Ten Hag ambaye anadaiwa kuwa mmoja ya mastraika anaotamani wasajiliwe.

Mkataba wa fundi huyu unamalizika mwisho wa mwaka 2026 hivyo ikiwa Man United itatuma ofa basi itatakiwa iwe ofa nono ili kuwashawishi Juventus kumuuza.

Ingawa hali ya uchumi na kiwango cha Juventus kwa sasa kinatoa asilimia nyingi pia za kwamba staa huyo huenda akaomba kuondoka ikiwa Man United itaonyesha nia kwani kueleka msimu ujao Juventus ina nafasi ndogo ya kushiriki Ligi ya Mabingwa kutokana na nafasi iliyokuwepo baada ya kunyang'anywa alama.

Kylian Mbappe Ingawa ni ngumu kutokana na mkataba wake kuwa bado mrefu lakini ishara za hivi karibuni zimeleta matumaini kwamba staa huyo huenda akatua Old Trafford katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi au mwakani.

Moja kati ya sababu zinazotajwa ni waarabu wanaotaka kuinunua Man United kuwa na uhusiano wa karibu na mabosi wa PSG, hivyo kama wakifanikiwa kuichukua timu huenda ikawa rahisi kuwashawishi wawauzie.

Vilevile hivi karibuni Mbappe aliwapongeza  Jadon Sancho na Murcus Rashford baada ya Sancho kuweka picha kwenye ukurasa wake wa Instagram ikiwaonyesha yeye na Rashford wameshika kombe, Mbappe akaandika:"Ni jambo zuri kuwaona mkiwa na furaha tena."

Hii imezua maswali mengi na kuonyesha kuwa ukaribu huo huenda ukahamia Carrington katika siku zijazo.

Chanzo: Mwanaspoti