Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United inauzwa, hauzwi!

Man United Gtsr Man United inauzwa, hauzwi!

Sat, 1 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Manchester United ipo kwenye hali ya sintofahamu tangu mwaka huu wa 2023 ulipoanza. Familia ya Glazer inayomiliki klabu hiyo bado haijaweka wazi kama inataka kuipiga bei timu hiyo jumla - au kuleta wawekezaji watakaotoa nafasi ya wao kuendelea kuwa na umiliki wa timu hiyo.

Familia hiyo ya kitajiri ya Marekani imekuwa na uhusiano wa hovyo na mashabiki wa Man United tangu walipoinunua klabu hiyo yenye maskani yake Old Trafford mwaka 2005. Novemba mwaka jana, familia hiyo ilibainisha kwamba inafikiria kuipiga bei klabu hiyo, kitu ambacho kiliamsha furaha kubwa kwa mashabiki wasiowapenda.

Lakini, tangu wakati huo mambo yamekuwa yakiibuka na kufifia, huku kukiwa hakuna maendeleo yoyote ya kuhusu kufikia mwafaka wa klabu hiyo kuuzwa. Wanunuzi wamejitokeza, ambapo tangu Januari mwaka huu, bilionea Mwingereza, Jim Ratcliffe alitangaza dhamira yake ya kuinunua klabu hiyo.

Ilipofika Februari, bosi mwingine siriazi aliibuka kutaka kuwa mmiliki wa timu hiyo, tajiri mfanyabiashara wa Qatar. Kulikuwa na tajiri mwingine pia, aliyefahamika kama Thomas Zilliacus naye alikuja na mpango wa kuinunua timu hiyo kwa maana ya kutaka kuungana na wenzake kuimiliki kwa pamoja Man United.

Kwa ofa zilizofika mezani kutakana kuinunua timu hiyo, tajiri Ratcliffe anahitaji kuwa na hisa nyingi, lakini si zote, wakati bilionea wa Qatar, Sheikh Jassim anahitaji kuimiliki Man United kwa asilimia 100.

Kampuni ya Raine Group ndiyo iliyopewa dhamana ya kupitia mchakato wa kuipiga bei klabu hiyo. Juni 7, ilielezwa kwamba Sheikh Jassim bin Hamad Al Thani alipeleka ofa yake ya tano ya kuinunua klabu hiyo jumla.

Na hapo, Sheikh Jassim alitoa okomo kwamba hadi kufika Juni 9 kama hakutakuwa na makubaliano yoyote, basi anajiondoa kwenye mchakato. Huko nyuma, familia ya Glazer yenye watoto sita, Avram, Bryan, Darcie, Edward, Joel na Kevin iliweka okomo wa kupokea ofa kuwa ni Aprili 28 na hadi kufika wakati huo, matajiri waliokuwa siriazi kwenye kuimiliki Man United, Sheikh Jassim kupitia Qatari Group na Sir Jim Ratcliffe kupitia kampuni yake ya INEOS waliwasilisha ofa zao mezani.

Sheikh Jassim ofa yake ilikuwa Pauni 5 bilioni, huku akidai pia atafanya marekebisho makubwa ya miundombinu kwenye timu hiyo na kulipa madeni yote atakapokuwa mmiliki.

Jambo hilo liliwafanya mashabiki kupendezwa na ofa ya Sheikh Jassim. Ratcliffe ofa yake na kampuni ya INEOS ofa yake ni kuimiliki Man United kwa asilimia 69, huku akitaka kuwaruhusu Joel na Avram Glazer kuendelea kuwa wamiliki wa timu hiyo wakiwa na hisa asilimia 20.

Lakini, kuna ripoti nyingine inadai kwamba Joel na Avram ambao ndio hasa wamekuwa karibu sana na Man United, wanaamini watapata pesa kutoka sehemu nyingine kuwasaidia katika kuendeesha timu hiyo na si kuiuza ili wabaki, wakiamini thamani ya klabu hiyo itafikia Dola 12.4 bilioni miaka 10 ijayo. Sheikh Jassim na Ratcliffe wamebaki kwenye mchuano wa kutaka kuinunua klabu hiyo sasa, huku Thomas Zilliacus akidai bado yupo kwenye mchakato.

Machi 16 na 17, Ratcliffe na Sheikh Jassim kila na mmoja na wakati wake walitembelea Old Trafford na kuzungumza na mkurugenzi mtendaji mkuu, Richard Arnold na madalali wengine.

Rekodi za hesabu za fedha za klabu hiyo kwa siku za karibuni haziwezi kuvutia wanunuzi wengi, ambapo deni la Man United liliripotiwa kufikia Pauni 535.7 milioni, huku mapato ya timu yakishuka kwa asilimia 10 kwa hesabu zinazoishia mwaka 2022. Rekodi za mwaka huu zinadai kwamba Man United imepata mapato kati ya Pauni 640 milioni.

Kuuzwa Man United shida iko wapi? Tangu Novemba 2022, familia ya Glazer ilitoa tangazo kwamba wanafikiria kuipiga bei klabu ya Man United. Lakini, kuchelewa kwa mchakato huo kumeanza kuwapa shida mashabiki.

Awali ilielezwa kwamba wanafamilia ya Glazer wamiliki wa klabu hiyo walikuwa wakitofautiana mambo kidogo, juu ya uamuzi wa pamoja kama timu ipigwe bei jumla au kwa hisa chache.

Joel na Avram walidai kwamba thamani ya klabu hiyo ni Pauni 6 bilioni. Sheikh Jassim na Sir Jim Ratcliffe wote ofa zao zilikaribia thamani hiyo, ikielezwa iliwekwa mezani ofa ya Pauni 5.5 bilioni.

Lakini, hadi sasa hakuna zabuni yoyote iliyotangazwa kushinda mchakato huo. Na sasa, imeibuka kwamba Joel na Avram wanachelewesha mchakato makusudi, kwa sababu hawana njia ya msingi ya kuuza timu hiyo, wakiamini baada ya miaka 12 ijayo, thamani ya Man United itafikia Dola 12.4 bilioni na hapo watapiga mkwanja wa kutosha.

Bei inapandishwa kila kukicha Kwa mujibu wa Financial Times, thamani ya Man United ni kati ya Dola 3.5 bilioni, licha kuna wakati ikikadiliwa kuwa Dola 4 bilioni. Lakini, familia ya Glazer ikaithaminisha Man United kwa kuwa Dola 6 bilioni. Wanaotaka kuinunua klabu hiyo hawajakubaliana na thamani hiyo.

Wameweka mzigo mezani, lakini wanandugu wawili, Joel na Avram Glazer wanaamini thamani ya Man United inakua na itafikia Dola 12.4 bilioni na hicho ndicho kinachochelewesha mchakato mzima wa kupigwa bei timu hiyo, ambapo Sheikh Jassim na Sir Jim Ratcliffe wanasubiri ni nani ataibuka mshindi.

Mashabiki waingilia kati Kufuatia kudorora kwa mchakato huo wa Man United kupigwa bei, huku ikiwa haifahamiki mpango huo utakamilishwa linii ili timu iingie kwenye mchakato wa usajili, mashabiki wanaopinga umiliki wa familia ya Glazer kwenye klabu hiyo walifanya maandamano kwa kuzuia milango ya maduka huko Old Trafford juzi Jumanne, wakati jezi za msimu ujao za timu hiyo zilipozinduliwa.

Mashabiki hao walijaribu kuwasilisha ujumbe kwamba wanataka timu ipigwe bei na familia hiyo ya Glazer iondoke mara moja. Hii si mara ya kwanza kwa mashabiki kuandamana kupinga umiliki wa familia ya Glazer, ambapo tukio kama hilo liliwahi kufanyika huko nyuma na kusababisha mechi kuashirishwa.

Maandamano ya juu ni kushinikiza wamiliki hao kurahakisha kuwauzia watu wengine timu, huku wakiamini ujio wa mabosi wapya utaifanya timu kuwa na pesa za ziada kwenye usajili baada ya sasa kuripotiwa kuwa na bajeti ya Pauni 100 milioni pekee.

Man United kwa sasa inabanwa na FFP (Financial Fair Play), hivyo usijili mpya ni lazima iuze kwanza, lakini kama watakuwa chini ya mmiliki mpya kati ya Sheikh Jassim au Sir Jim Ratcliffe basi watakuwa na ruhusu ya kufanya usajili kutokana na ruhusa inayotolewa kwa mmiliki mpya kuboresha timu yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: