Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United hali tete, wachezea kichapo kwa West Ham

IMG 4057.jpeg Man united wakishangaa kipigo cha West Ham

Mon, 8 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji West Ham United wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Jumapili Uwanja wa London.

Bao pekee la West Ham United limefungwa na mshambuliaji Mualgeria, Mohamed Saïd Benrahma aliyemtungua kipa David de Gea kwa shuti la umbali wa mita 20 dakika ya 27.

Kwa ushindi huo, West Ham United ya kocha David Moyes inafikisha pointi 37 katika mchezo wa 35, ingawa inabaki nafasi ya 15, wakati Manchester United inabaki na pointi zake 63 za mechi 34 nafasi ya nne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: