Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United bado ina imani na Ten Hag

'Huu Ni Mwisho Wa Ten Hag   Hakuna Kurudi Nyuma' Man United bado ina imani na Ten Hag

Tue, 3 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya changamoto zinazojidhihirisha waziwazi, uongozi wa Manchester United unaonekana kuwa bado una imani na Kocha mdachi Erik Ten Hug.

Mtendaji Mkuu wa Manchester United, Omar Berrada, na Mkurugenzi wa Michezo, Dan Ashworth, wameeleza kuwa klabu inaendelea kumuunga mkono kikamilifu kocha Ten Hag.

Berrada alisema, “Erik ana uungwaji mkono wetu na tumefanya kazi kwa karibu sana pamoja katika dirisha hili la uhamisho. Tutaendelea kufanya kazi kwa karibu naye ili kumsaidia kupata matokeo bora kutoka kwa timu.”

Ashworth aliongeza kuwa, “Nimefurahia kufanya kazi na Erik kwa wiki nane zilizopita. Kazi yangu ni kumsaidia kwa kila njia ninayoweza ili aweze kujikita kikamilifu kwenye uwanja wa mazoezi na mpango wa kiufundi wa mechi ili kuleta mafanikio kwa Manchester United.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live