Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United bado Majanga, yakubali kichapo

Everton Nnnnnn Everton yaichapa Man United 1-0

Sat, 9 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Everton imefufua matumaini ya kuweza kubaki Ligi Kuu (EPL) baada ya ushindi wa goli 1-0 mbele ya Manchester United.

Ushindi wa Everton mbele ya Manchester United kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa jioni ya leo una maana kubwa kwao kwa kuwa hawakuwa wanachohitaji zaidi ya pointi tatu.

Bao la ushindi kwa Everton limepachikwa na Anthony Gordon ilikuwa ni dakika ya 27 na kuifanya timu hiyo kubakiza pointi tatu nyumbani katika Uwanja wa Goodison Park.

Sasa Everton inafikisha pointi 28 ikiwa nafasi ya 17 kwenye msimamo huku United ikibakiwa na pointi zake 51 ipo nafasi ya 7.

Matumaini ya kuweza kumaliza ndani ya Top 4 kwa United yanazidi kuwa magumu kutokana na mwendo wa matokeo kuwa toauti na vile ambavyo wengi wanafikiria.

Manchester United iliweza kupiga jumla ya mashuti 12 huku mashuti manne pekee yakilenga lango na ni mashuti 7 yalipigwa na Everton huku matatu pekee yakilenga lango kwenye mchezo wa leo ambao United waliongoza kwenye suala la umiliki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live