Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United, Zirkzee kitu kitamu kinapikwa

Joshua Zirkeee Joshua Zirkzee

Wed, 26 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Manchester United imeripotiwa kujifungia kwenye mazungumzo na mawakala wa straika Joshua Zirkzee.

Kwenye mchakato wa kunasa saini ya mchezaji huyo, Man United ipo tayari kulipa Pauni 34 milioni ambazo Bologna imezibainisha kwenye mkataba wa mchezaji huyo kwa timu itakayohitaji saini yake, ilipe imbebe jumla.

Zirkzee ameibuka kuwa kipaumbele kwenye mpango wa usajili wa Man United katika kuboresha safu ya ushambuliaji ili kuja kusaidiana na Rasmus Hojlund, kufanya safu hiyo ya ushambuliaji ya kikosi cha Erik ten Hag kuwa na makinda matata.

Zirkzee atakwenda kuongeza kitu kwenye fowadi ya timu hiyo ya Old Trafford, ambayo kwenye dirisha hili imempoteza Anthony Martial.

Arsenal huko nyuma iliwahi kuhusishwa na Zirkzee baada ya kukwama kwenye usajili wa straika wa Slovenia, Benjamin Sesko, ambaye aliamua kusaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki RB Leipzig.

Zirkzee, 23, kwenye mkataba wake kuna kipengele kinachobainisha kwamba timu itakayohitaji saini yake, inapaswa kulipa Euro 40 milioni (Pauni 34 milioni). Lakini, kila kitu kitabaki kwa Zirkzee kuamuya, huku miamba ya Italia, AC Milan nayo ikijiandaa kulipa kiasi hicho cha pesa ili kumbakiza mchezaji huyo kuendelea kukipiga kwenye Serie A.

Straika huyo mwenye kimo cha futi 6 na inchi 4 alifunga mabao 11 na asisti nne kwenye mechi 34 alizocheza kwenye Serie A msimu uliopita.

Thamani yake sokoni ni Pauni 50 milioni, hivyo kama bosi wa Man United, bilionea Sir Jim Ratcliffe akimnasa kwa pesa iliyotajwa kwenye mkataba wake, Pauni 34 milioni itakuwa bei ya chini sana.

Man United ilimnasa straika Hojlund mwaka jana kutokea Atalanta kwa ada ya Pauni 72 milioni. Zirkzee yupo kwenye kikosi cha Uholanzi kinachoshiriki fainali za Euro 2024 huko Ujerumani. Wakala wake Kia Joorabchian anahitaji ada ya uwakala ya Pauni 12.6 milioni.

Chanzo: Mwanaspoti