Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United: Tutawapiga Man City

Ten Hag With Ferguson Man United: Tutawapiga Man City

Tue, 30 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Manchester United, Eric Ten Hag (53) raia wa Uholanzi ametamba wapinzani wao Manchester City hawatotoka katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho England (FA Cup) utakaopigwa Jumamosi ijayo Juni 03, 2023 katika uwanja wa Wembley.

Ten Hag ametoa kauli hiyo siku ya jana katika uwanja wa nyumbani wa United, Old Trafford mbele ya halaiki ya mashabiki wake mara baada ya kumalizika mchezo wao wa kutamatika Ligi Kuu nchini England EPL 2022/23 kwa kuifunga Fulham (2-1).

"Tumesaliwa na mchezo mmoja tu mbeleni, na nina hakika wachezaji hawa kikosini watawawapa kila kitu kuhakikisha wanawafunga City katika mchezo wa juma ijayo uwanja wa Wembley. "

Ten Hag ameongeza kuwa washabiki wawe na imani na kikosi chao kwani wamejiandaa kuwakabili City na kuhakikisha kombe lina salia Old Trafford.

United imemaliza EPL 22/23 katika nafasi ya tatu ikiwa na jumla ya alama 75 katika michezo 38 ya ligi hiyo na kujihakikishia kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Ulaya UEFA msimu ujao.

Itakumbukwa mafanikio makubwa ya Ten Hag tangu ajiunge na wababe hao msimu huu ni kutwaa Kombe la Ligi (Carabao Cup).

Hata hivyo mioyo ya washabiki wengi wa United ni kuwa na imani na Kocha huyo ambaye anatazamiwa kuwa na mafanikio makubwa siku za usoni na kuwa mrithi rasmi wa nguli wa United Kocha mstaafu Sir Alex Ferguson aliyetundika daruga mwaka 2013 akiwa amedumu klabuni hapo kwa miaka 37 tangu kutambulishwa rasmi 1986.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: