Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United, Liverpool vita kali Kombe la FA

Diaz X Anthony .jpeg Man United, Liverpool vita kali Kombe la FA

Sun, 17 Mar 2024 Chanzo: Mwananchi

Manchester United inaweza kukubali au kukataa kuwa daraja la Liverpool katika harakati zake za kutwaa mataji manne msimu huu wakati timu hizo zitakapokutana kwenye mechi ya robo fainali ya Kombe la FA leo kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Tayari Liverpool imetwaa kombe la Ligi baada ya kuifunga Chelsea kwa bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa Februari 25 mwaka huu.

Na sasa timu hiyo inayonolewa na Jurgen Klopp ina fursa ya kutwaa mataji ya Ligi Kuu England (EPL), Kombe la FA na lile la Europa lakini hapana shaka mchezo wa leo ni kigingi kigumu kwao katika kutimiza lengo lao.

Na hiyo ni kutokana na upinzani inaotarajia kuupata kutoka kwa Manchester United ambayo taji hilo la FA ndilo pekee ambalo ina uwezekano wa kulipata msimu huu baada ya kushindwa kutamba kwenye Ligi ya Mabingwa, Kombe la Ligi na ina matumaini finyu ya kutwaa EPL kwa msimu huu kwani imezidiwa pointi 17 na Arsenal inayoongoza msimamo wa ligi hiyo.

Shilingi inaonekana kusimama baina ya timu hizo kwani hakuna mojawapo ambayo imekuwa ikimuonea mwenzake pindi zikutanapo kwenye Kombe la FA na kuthibitisha hilo, kuanzia 2005 hadi sasa, zimekutana mara nne kwenye Kombe hilo na kila timu imeibuka na ushindi mara mbili.

Refa John Brooks ndiye atachezesha mechi hiyo ya leo akisaidiwa na Lee Betts na Timothy Wood huku mwamuzi wa nne/akiba akipangwa kuwa Anthony Taylor.

Manchester United ipo katika harakati za kulitwaa taji hilo kwa mara ya 13 ili iikaribie Arsenal ambayo inaongoza ikiwa imechukua ubingwa mara 14 wakati Liverpool yenyewe inasaka taji la tisa la mashindano hayo.

Kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, Chelsea nayo itakuwa ikisaka kusonga mbele kwenye mashindano hayo wakati itakapoikaribisha Leicester City.

Taji la FA ndilo pekee ambalo Chelsea inayoshika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England ina uwezekano wa kulichukua msimu huu ambapo ikifanya hivyo itakuwa imelitwaa kwa mara ya tisa.

Ikumbukwe droo ya hatua ya nusu fainali itachezeshwa leo mara baada ya kumalizika kwa mechi kati ya Man United na Liverpool.

Chanzo: Mwananchi