Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United, Chelsea, mechi ya heshima

Bruno Fernandes Vs Raheem Sterling Man United, Chelsea, mechi ya heshima

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ligi Kuu England inaendelea leo kwa michezo sita ukiwemo kati ya Manchester United na Chelsea , unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa mpira wa miguu.

Manchester United ipo nafasi ya saba katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 24 baada ya michezo 14 wakati Chelsea ni ya 10 ikikusanya pointi 19.

Katika michezo 78 ya mwisho timu hizo zilipokutana Manchester United imeshinda mara 23, zimetoka sare mara 32 wakati Cheslea imeshinda mara 23.

Michezo mingine ya EPL leo pamoja na Ligi Kuu Ufaransa ni kama ifuatavyo:

PREMIER LEAGUE

Brighton vs Brentford

Crystal Palace vs Bournemouth

Fulham vs Nottigham Forest

Sheffield United vs Liverpool

Aston Villa vs Manchester City

LIGUE 1

Marseille vs Lyon.

MATOKEO YA JANA

Wolves 1-0 Burnley

Luton 3-4 Arsenal

Goli la dakika za lala salama la Declan Rice liliwapatia Arsenal alama zote tatu na kuendelea kujichimbia kileleni kwa pointi tano zaidi kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live