Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United, Bayern jino kwa jino kwa Palhinha

Arsenal Na Chelsea Kwenye Mbio Kumsaka Nyota Wa Fulham Joao Palhinha Joao Palhinha

Sun, 16 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Machester United inataka kuipiku Bayern Munich kwenye dili la kuiwania saini ya kiungo wa Fulham, Joao Palhinha dirisha hili.

Bayern ndio ilikuwa ya kwanza kuiwania saini ya staa huyu tangu mwaka jana lakini ilishindikana, hivyo bado inapambana kuhakikisha wanafanikisha hilo kwa sasa.

Man United inamwangalia Palhinha kama mbadala wa Casemiro ingawa inaweza kuwagharimu pesa nyingi kumpata kwa kuwa hawatoshiriki Ligi ya Mabingwa mwakani.

Bayern ambayo inapambana nayo kwenye vita hiyo ina nafasi ya kumshawishi zaidi Palhinha kwa sababu ya kufuzu kucheza michuano hiyo.

Mabosi wa Fulham wameripotiwa kutaka ofa isiyopungua Pauni 50 milioni ili kumuuza kiungo huyu mwenye umri wa miaka 28, ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2028. Msimu huu amecheza mechi 39 za michuano yote.

MANCHESTER City imeendelea kusisitiza haina mpango wa kumuuza wala kumtoa kwa mkopo mshambulaji wao Julian Alvarez dirisha hili na timu kibao zimeonyesha nia ya kumsajili ikiwamo Atletico Madrid iliyohitaji kumchukua hata kwa mkopo. Msimu uliopita Alvarez alicheza mechi 54 za michuano yote na kufunga mabao 19 na mkataba wake unamalizika mwaka 2028.

ATHLETIC Bilbao imeiambia Arsenal itatakiwa kutoa Euro 50 milioni ili kuipata saini ya winga wao raia wa Hispania, Nico Williams, 21, dirisha hili. Nico ambaye amekuwa akiwindwa na Arsenal kwa muda mrefu, msimu uliopita alicheza mechi 37 za michuano yote na kiasi hicho cha pesa ndicho kipo kwenye mkataba wake. Arsenal ya Kocha Mikel Arteta inataka kuendeleza moto wake msimu ujao na inajipanga kuanzia kwenye usajili.

NEWCASTLE imewasiliana na AC Milan kuulizia uwezekano wa kuipata huduma ya beki wa timu hiyo raia wa England Fikayo Tomori, 26, dirisha hili la majira ya kiangazi. Tomori ambaye ni mmoja kati ya wachezaji tegemeo wa Milan, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Msimu uliopita alicheza mechi 35 za michuano yote.

TAARIFA za uhakika kutoka Sky Sports zinadai kuna timu moja inayoshiriki Ligi ya Mabingwa imetuma ofa ya kutaka kumsajili kiungo wa Everton, Amadou Onana dirisha hili. Licha ya taarifa hizo za Sky kutoweka wazi ni timu gani, kwa mujibu wa tovuti ya Toffeweb, Arsenal ndiyo imewasilisha ofa hiyo. Mkataba wa sasa wa Onana unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.

AC Milan inataka kulipa Pauni 20 hadi 25 milioni kwa ajili ya kumsajili beki wa kulia wa Aston Villa na Poland, Matty Cash, 26, dirisha hili. Kwa mujibu wa tovuti ya Athletic, Villa inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 30 milioni ili kumuuza Cash ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2027. Milan imevutiwa na kiwango cha Cashalichoonyesha ndani ya England na kwenye michuano ya kimataifa msimu uliopita.

JUVENTUS imeendelea kuishawishi Manchester United ikubali kumwachia mshambuliaji wao Mason Greenwood iliyotaka kumchukua tangu dirisha la majira ya baridi mwaka jana lakini ilishidikana. Greenwood aliyecheza kwa mkopo Getafe msimu uliopita, alionyesha kiwango bora kilichovutia timu nyingi. Juventus imewasilisha ofa ya Pauni 40 milioni.

REAL Madrid bado inasubiria majibu kutoka kwa Tottenham juu ya ombi lao la kutaka kumsajili beki wa timu hiyo Cristian Romero dirisha lijalo. Mabosi wa Madrid wameamua kuhamia kwenye eneo la ulinzi na wanataka kuboresha baada ya kufanikiwa kwenye eneo la ushambuliaji ilipomshusha Kylian Mbappe. Mkataba wake unamalizika mwaka 2027.

Chanzo: Mwanaspoti