Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man U majanga, yachapwa 4, rekodi yavunjwa

Leicester United Wachezaji wa Leicester City wakishangilia moja ya magoli yao

Sat, 16 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashetani wekundu, Manchester United leo wamekwenda kucheza mechi ya tatu mfululizo ya Ligi kuu England pasipo kupata matokeo ya ushindi mara baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-2 kutoka kwa Leicester City.

Kipigo hicho walichokitoa Leicester, kinamaliza ubabe wa Man United kucheza mechi 29 ugenini pasipo kupoteza.

Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford amefunga goli katika mchezo wake wa kwanza msimu huu likiwa la kusawazisha mara baada ya kuwa nyuma na kufanya matokeo kuwa 2-2.

Dakika 7 za mwisho Leicester waliamka na kufunga magoli ya haraka likiwemo la dakika za lala salama lililofungwa na Jamie Vardy.

Matokeo hayo yanaacha presha kubwa kwa mwalimu wa United Ole Gunner Solkjaer kwa namna ambavyo kikosi hicho kinakwenda, wakati washindani wengine wa Taji la Ligi kuu wanaimarika kila siku wakiwemo LLiverpool na Man City.

Goli jingine la Man United limefungwa na Mason Greenwod 19', wakati yale ya Leicester yamefungwa na Youri Tielemans 31', Caglar Soyuncu 78', Jamie Vardy 83 na Patson Daka 91.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live