Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man U kuanza uchunguzi chanzo cha majeruhi

Erik Ten Hag Manchester United September 2023 1 Kocha wa Man United, Erik Ten Hag

Sun, 15 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa michezo wa Manchester United John Murtough amesema wanatarajia kuanza kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha wachezaji wao asilimia kubwa kupata majeraha msimu huu.

Kwa sasa takribani wachezaji sita (6) wa kikosi cha kwanza wana majeraha yatakayowafanya wakae nje kwa muda mrefu akiwemo Luke Shaw, Lisandro Martinez, Tyrel Malacia, Aaron Wan-Bissaka, Amad Diallo na Kobie Maino, wengine waliokosekana kwa muda sasa ni Raphael Varane, Sergio Reguilon na Mason Mount.

Casemiro nae huenda akakosekana katika michezo kadhaa baada ya kupata majeraha wakati anaitumikia timu yake ya Taifa ya Brazil.

Kwa ujumla sasa Manchester United ina majeruhi 16 kwenye kikosi chao hadi hivi sasa.

Unadhani tatizo la Manchester United ni nini?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live