Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man City yawaenzi magwiji wake

Man City Magwijis Man City yawaenzi magwiji wake

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Manchester City imezindua kumbukumbu ya kudumu ya sanamu mpya ya magwiji watatu wa klabu hiyo ambao ni Colin Bell, Francis Lee na Mike Summerbee.

Sanamu hizo zilizoundwa kwa shaba nje ya Uwanja wa Etihad ni kumbukumbu ya utumishi wa nyota hao wa jumla ya miaka 30 pamoja na kusherehekea mafanikio ya klabu hiyo mwishoni mwa miaka ya 1960 na mwanzoni mwa miaka ya 1970.

Katika kuenzi mafanikio yao ambapo Man City ilitwaa ubingwa wa Ligi Daraja la Kwanza, Kombe la FA, Kombe la Ligi na Kombe la Washindi wa Kombe la Ulaya, majina ya wachezaji wote 29 waliochangia kipindi hicho yameandikwa kwenye sahani ya shaba kwenye sanamu hilo.

Summerbee alikuwa wa kwanza kuwasili Manchester mnamo 1965, akifunga mabao 67 katika mechi 449 kwa kipindi cha muongo mmoja wa utumishi wake klabuni hapo.

Colin Bell, almaarufu ‘Mfalme wa Kippax’ aliifungia Man City mabao 153 katika michezo 498 katika kipindi cha miaka 13 katika klabu hiyo huku Francis Lee aliyetua klabuni mwaka 1967 akifunga mabao 148 katika michezo 330.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live