Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man City yashusha dozi nzito kwa Leeds, yapiga goli 7

Kdb Score Kevin De Bruyne alifunga bao mbili katika ushindi wa goli 7

Wed, 15 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi wa EPL, Manchester City wameendeleza ubabe katika Ligi Kuu ya England baada ya kuichapa Leeds United mabao 7-0 usiku wa jana Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.

Mabao ya Man City yamefungwa na Phil Foden dakika ya nane, Jack Grealish dakika ya 13, Kevin De Bruyne mawili dakika ya32 na 62, Riyad Mahrez dakika ya 49, John Stones dakika ya 74 na mtokea benchi, Nathan Ake dakika ya 78.

Kwa ushindi huo, Man City inafikisha pointi 41 katika mchezo wa 17 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi nne zaidi ya Liverpool ambayo pia ina mechi moja mkononi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live