Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man City yampiga mtu bao 6, Doku atakata

Manchester City.jpeg Man City yampiga mtu bao 6, Doku atakata

Sat, 4 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Manchester City imefanikiwa kupata alama tatu kwa kishindo baada ya kuibamiza Bournamouth mabao 6-1, Huku winga Jeremy Doku akitakata.

Manchester City wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wamepata alama tatu muhimu kwa ushindi wa kishindo mbele ya Bournamouth na kuwafanya kwenda kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.

Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Uingereza walifanikiwa kuanza mchezo huo kwa kasi ambapo ndani ya kipindi cha kwanza walipata mabao matatu ambayo yaliwapa uongozi wa mchezo huo.

Kipindi cha pili klabu hiyo iliendelea ilipoishia ambapo walifanikiwa kupata mabao mengine matatu, Huku winga Jeremy Doku usajili mpya ndani ya klabu hiyo akitakata kwelikweli baada ya kufunga bao moja na kupika mabao manne.

Mabao ya Manchester City yalifungwa Jeremy Doku, Bernardo Silva mabao mawili, Akanji, Nathan Ake, pamoja na Phil Foden na kuwafanya Man City kufikisha alama 27, Lakini stori kubwa ni uwezo ambao ameuonesha Jeremy Doku katika mchezo wa leo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live