Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man City yamkaribisha rasmi Gerrard EPL, yaichapa Aston Villa 2-1

City Man Beki wa Manchester City, Ruben Diaz akishangilia goli la ufunguzi

Thu, 2 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Manchester City wameendeleza mawindo yao ya ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya kuichapa Aston Villa 2-1 usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Etihad.

Mabao ya Manchester City yalifungwa na Ruben Dias dakika ya 27 na Bernardo Silva dakika ya 43, wakati la Aston Villa lilifungwa na Ollie Watkins dakika ya 47.

Hiki ni kipigo cha kwanza kwa Kocha mpya Aston Villa, Steven Gerrard tangu achukue majukumu ya kukionoa kikosi hicho mwezi uliopita.

Manchester City inafikisha pointi 32 baada ya ushindi huo, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na Chelsea inayoongoza baada ya timu zote kucheza mechi 14, wakati Aston Villa inabaki na pointi zake 16 za mechi 14 pia katika nafasi ya 13.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live