Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man City yakwaa kisiki Ubingwa wa EPL

Man City Vs Nottigham.jpeg Man City kwa sare hiyo wametoa fursa kwa Arsenal kuendelea kusalia kileleni

Sun, 19 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Manchester City imelazimishwa sare na klabu ya Nottingham Forest katika mchezo wa ligi kuu ya kuu ya England katika mchezo uliopigwa katika dimba la City Ground.

Klabu ya Manchester City ambayo katikati ya wiki ilifanikiwa kuwafunga vinara wa ligi kuu ya Uingereza klabu ya Arsenal kwa mabao matatu kwa moja, Lakini mchezo wa jana wamekutana na kizingiti baada ya klabu ya Nottingham Forest kuwalazimisha sare ya bao moja kwa moja.

Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Uingereza walifanikiwa kuutawala mpira kuanzia dakika ya kwanza ya mchezo na kutengeneza nafasi kadhaa, Dakika ya 41 ya mchezo mchezaji Bernardo Silva alipiga shuti kali lililoipa bao la uongozi klabu hiyo na mpaka kwenda mapumziko walikua na uongozi wa bao moja kwa bila.

Manchester City walirejea kipindi cha pili wakiendelea kutafuta mabao zaidi wakijaribu kutengeneza nafasi ambazo hazikuzaa mabao mpaka pale dakika ya 84 Chris Wood akiipatia bao la kusawazisha klabu ya Nottingham Forest na mpaka mpira unamalizika matokeo yalikua 1-1.

Klabu ya Manchester City baada ya kutoka sare katika mchezo wa jana na kudondosha alama mbili katika mchezo huo, Sasa wamefikisha jumla ya alama 52 wakiwa nyuma ya vinara klabu ya Arsenal kwa tofauti ya alama mbili kwani Arsenal wao wameshinda mchezo wao dhidi ya Aston Villa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live