Manchester City imetengeneza historia ya kubeba makombe matatu baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Inter Milan kwenye fainali ya Ligi Mabingwa Ulaya bao hilo liliwekwa kimiani na Rodri.
Manchester United ndio timu pekee iliyokuwa ikishikilia rekodi ya kubeba makombe matatu ya Ligi Kuu, Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu mmoja miaka 24 iliyopita.
Man City imeibuka na kufikia rekodi hiyo iliyowekwa na Sir Alex Ferguson mwaka 1999 kabla ya kuitema Man United mwaka 2013 baada ya kuipa ubingwa wa Ligi Kuu England.
Kikosi cha Pep Guardiola kilifanikiwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Mabingwa Ulaya jijini Istanbul, Uturuki wiki moja tu baada ya kunyakuwa Kombe la FA.
Baada ya kutolewa kwa kishindo katika nusu fainali ya mwaka jana dhidi ya Real Madrid ilipofunga mabao mawili dakika za mwisho na mpira ikalazimika kwenda katika dakika za nyongeza Los Blancos ikaibuka kidedea.
Man City imelipiza kisasi msimu huu kwa kuiondoa Madrid kwa mabao 4-0 uwanja wa Etihad katika nusu fainali ya pili ya michuano hiyo. Nusu fainali ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 Santiago Bernabeu.
Man City walipata taji lao la pili wiki moja kabla ya fainali hiyo ya Ligi Mabingwa Ulaya dhidi ya wapinzani wao Man United uwanja wa Wembley.