Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man City yaichapa Leicester kwa mbinde

KDB Score 1 Kiungo wa Man City alifunga bao la Man City

Sun, 30 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bao pekee la Kevin De Bruyne dakika ya 49 jana liliipa Manchester City ushindi wa 1-0 dhidi ya Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa King Power, Leicester, Leicestershire.

Kwa ushindi huo, kikosi cha Pep Guardiola kinarejea kileleni japo kwa muda kufuatia kufikisha pointi 29 katika mchezo wa 12, wakiizidi pointi moja Arsenal ambayo ina mechi moja mkononi.

Hali bado si nzuri kwa kocha Brendan Rodgers, kwani baada ya kichapo hicho wanabaki na pointi zao 11 za mechi 13 sasa nafasi ya 18 kwenye ligi ya timu 20, ambayo mwisho wa msimu tatu zitashuka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live