Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man City yaichapa Fulham 4-1, Kombe la FA

City Vs Fulham Man City wakishangilkia goli dhidi ya Fulham

Sun, 6 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Manchester City imeshinda bao 4-1 dhidi ya timu ya Championship Fulham katika mchezo wa Kombe la FA England mchezo uliopigwa dimba la Etihad Leo Jumamosi Februari 5.

Ushindi wa Man City unaifanya kufuzu kucheza raundi ya tano ya Kombe hilo ambapo magoli mawili ya winga wa kimataifa wa Algeria Riyad Mahrez na yale ya Ilikay Gundogan na John Stones yamewapa ushindi mjarabu kuelekea hatua hiyo.

City, ambao wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu England kwa tofauti ya alama tisa na timu iliyo nafasi ya pili huku wakiwa hawajapoteza mchezo wowote ule wa mashindano ya nyumbani tangia mwezi Octoba 2021 iliduwazwa na goli la mapema la Fabio Carvalho kupitia krosi ya Harry Wilson.

Kupata goli tu Etihad siyo jambo rahisi maana hata klabu za EPL ni timu tatu tu ambazo msimu huu zimefunga goli katika uwanja huo, moja kati ya hizo iliibuka na ushindi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live