Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man City yaendeleza presha kwa Arsenal, yaichapa Leeds 3-1

Leeds Vs Man City Man City yaendeleza presha kwa Arsenal, yaichapa Leeds 3-1

Thu, 29 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Manchester City imeendeleza ubora wake huku mshambuliaji wa timu hiyo Erling Haaland akiwa katika ubora wa hali ya juu pia kufuatia kuisaidia kuibuka na ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Leeds United mchezo wa Ligi Kuu England mtanange uliopigwa uwanja wa Elland Road Jumatano.

Kwenye mchezo huo, Haaland nyota wa kimataifa wa Norway alifunga mabao mawili yote yakitengenezwa na Jack Grealish ingawa bao la kwanza kwa City lilifungwa na Rodri dakika moja kabla ya mpira kwenda mapumziko.

Bao la kufutia machozi kwa Leeds United limefungwa na Paschal Struijk nyota wa Uholanzi dakika ya 73.

Kwa matokeo hayo, Manchester City inarudi nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi tano dhidi ya vinara Arsenal kwenye msimamo wa Ligi Kuu England huku wasumbufu Leeds wakishika nafasi ya 15 wakiwa na alama 15.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live