Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man City warudi kileleni EPL

Sthnh Man City warudi kileleni EPL

Sat, 21 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi, Manchester City FC wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Brighton & Hove Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.

Mabao ya Manchester City yamefungwa na washambuliaji wake, Muargentina Julián Álvarez dakika ya saba na Mnorway, Erling Haaland dakika ya 19, wakati bao pekee la Brighton & Hove Albion limefungwa na kinda wa Hispania, mzaliwa wa Guinea-Bissau, Ansu Fati dakika ya 73.

Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 21 na kupanda kileleni mwa ligi hiyo ikiizidi pointi moja Liverpool, wakati Brighton & Hove Albion inabaki na pointi zake 16 nafasi ya saba baada ya wote kucheza mechi tisa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live