Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man City wapokea kichapo EPL

F8560046 0AA2 4991 972C FF0B41D525E3.jpeg Man City wameachwa alama 5 na Arsenal wanaoongoza Ligi

Sun, 13 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi, Manchester City jana wamechapwa mabao 2-1 na Brentford FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.

Pongezi kwa mshambuliaji wa England, Ivan Toney aliyeifungia mabao yote Brentford FC dakika ya 19 na 90 na ushei, wakati bao pekee la Man City lilifungwa na Phil Foden dakika ya 45 na ushei.

Kwa ushindi huo, Brentford FC inafikisha pointi 19 katika mchezo wa 15 na kusogea nafasi ya 10, wakati Man City inabaki na pointi zake 32 katika nafasi ya pili, ikizidiwa pointi mbili na Arsenal baada ya wote kucheza mechi 14.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live