Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man City waichapa Copenhagen goli 3

IMG 8834.jpeg Man City waichapa Copenhagen goli 3

Wed, 14 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi, Manchester City jana wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, huku FC Copenhagen katika mchezo wa kwanza Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Parken Jijni Copenhagen, Denmark.

Mabao ya Manchester City yamefungwa na Kevin De Bruyne dakika ya 10, ' Bernardo Silva dakika ya 45 na Phil Foden dakika ya 90 na ushei, wakati la Copenhagen limefungwa na Magnus Mattsson dakika ya 34.

Timu hizo zitarudiana Machi 6 Uwanja wa Etihad Jijini Manchester na mshindi wa jumla atakwenda Robó Fainali.

Mechi nyingine ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa jana, Real Madrid waliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, RB Leipzig bao pekee la Brahim Díaz dakika ya 48 Uwanja wa Red Bull Arena Jijini Leipzig.

Nao watarudiana Machi 6 Uwanja wa Santiago Bernabéu Jijini Madrid na mshindi wa jumla atakwenda Robo Fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live