Imefahamika kuwa Mabingwa wa Soka nchini England Manchester City, wameanza mikakati ya kumnasa kiungo wa Borussia Dortmund, Jude Bellingham ili kumsajili kwa msimu ujao wa 2023/24,
Man City inatajwa kuwa katika mawindo ya kumnasa Kiungo huyo kutoka England tangu mwezi Oktoba mwaka jana kwa mujibu wa ripoti.
Imeelezwa kiungo huyo alialikwa katika vyumba vya kubadilishia nguo baada ya kupata suluhu dhidi ya Manchester City, timu hizo zilipomenyana kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita 2021/22.
Kocha Pep Guardiola baada ya kumsaini Erling Haaland katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi, Man City inajiamini itafanikiwa kuipata saini ya Bellingham atakayeuzwa kwa kitita cha Pauni Milioni 130.
Man City wanaamini kutokana na ukaribu wa Bellingham na Haaland itakuwa njia nzuri ya kumshawishi aungane na mchezaji mwenzake wa zamani wa Dortmund.
Wakati huo huo, Man United nayo imeingia katika kinyang’anyiro cha kuwania saini ya kiungo huyo wa kamataifa wa England.
Lakini ofa itakayotolewa na Man United itategemea na mazungumzo ya uhamisho wa nyota huyo kukamilika haraka iwezekanavyo katika dirisha la usajili la kiangazi.
Mabosi wa United wanaamini uhamisho wa Bellingham utakuwa mgumu kwasababu timu nyingi zita muwania.
Liverpool ilijitoa katika mbio za kuwania saini ya Bellingham, kwasababu wanadhani uhamisho wake utakuwa na mlolongo kwahiyo wataangalia viungo wengine watakaopatikana sokoni.