Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man City njie nyeupe Ubingwa EPL

Man City Vs Everton Wachezaji wa Man City wakishangilia ushindi siku ya jana

Mon, 15 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabinngwa watetezi, Manchester City wamejisogeza jirani mno na taji lingine la Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Everton Uwanja wa Goodison Park, Liverpool.

Mabao ya Manchester City yamefungwa na Nahodha, Ilkay Gundogan mawili dakika ya 37 na 51 na Erling Haaland dakika ya 39, ambalo linakuwa bao lake la 36 msimu huu.

Kwa ushindi huo, Manchester City wanafikisha pointi 85 katika mchezo wa 35 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi nne zaidi ya Arsenal akihitaji kushinda mchezo ujao dhidi ya Chelsea Mei 21 kutawazwa rasmi kuwa bingwa tena.

Kwa upande wao Everton baada ya kuchapwa leo wanabaki na pointi zao 32 za mechi 36 nafasi ya 17.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: