Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man City ni mwendo wa vichapo EPL

GettyImages 1237008498 Bernado Silva aliweka nyavuni magoli mawili

Sun, 5 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi kunako EPL, Klabu ya Manchester City imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kuichapa Watford mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Vicarage.

Mabao ya Manchester City yamefungwa na Raheem Sterling dakika ya nne ya mchezo na Kiungo wa Kireno, Bernardo Silva mawili dakika ya 31 na 63, wakati goli pekee la Watford limefungwa na mtokea benchi, Cucho Hernandez dakika ya 75.

Kwa ushindi huo, Man City ya kocha Pep Guardiola inafikisha pointi 35 na kupanda kileleni mwa ligi, ikiizidi pointi moja Liverpool inayofuatia na mbili Chelsea, wakati Watford inabaki na pointi zake 13 katika nafasi ya 17 baada ya timu zote kucheza mechi 15.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live