Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man City mambo magumu EPL, walazimishwa sare Etihad

City Vs Ev.jpeg Mchezo ulimalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1

Sun, 1 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi wa EPL, Manchester City wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Everton Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.

Mshambuliaji Mnorway, Erling Haaland alianza kuifungia Man City dakika ya 24 hilo likiwa bao lake la 27 la msimu, kabla ya Demarai Gray kuisawazishia Everton dakika ya 64.

Kwa matokeo hayo, Man City inafikisha pointi 36, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi saba na vinara, Arsenal baada ya wote kucheza mechi 16.

Kwa upande wao, Everton wanabaki na pointi zao 15 za mechi 17 nafasi ya 16.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live