Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man City kumuweka sokoni Grealish

Jack Grealish Man City kumuweka sokoni Grealish

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

City huenda ikamuachia winga wao raia wa England, Jack Grealish, 28, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi kwa ajili ya kupata pesa itakazozitumia kufanya usajili wa mastaa mbalimbali inaowahitaji katika dirisha lijalo.

Grealish amekuwa hapati nafasi ya kutosha kwenye kikosi cha kwanza cha Man City. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.

Staa huyu hajaonyesha kiwango kilichotarajiwa tangu kuanza kwa msimu huu na kocha wa Man City Pep Guardiola, alishawahi kutamka wazi kwamba haridhishwi na kiwango chake.

Kuna ripoti zinazoeleza kuwa Man City inataka kumsajili winga wa Napoli, Khvicha Kvaratskhelia katika dirisha lijalo ili akachukuwe nafasi ya Grealish.

Tangu dirisha lililopita kumekuwa na taarifa zinazomhusisha Grealish na Arsenal inayodaiwa kuandaa zaidi ya Pauni 50 milioni kwa ajili ya kufanikisha mchakato wa kumsajili.

Pep anawania taji la Ligi Kuu England analolishikilia na amekuwa akitumia wachezaji wanaompa matokeo kwani vita ya ubingwa ni kali mbele ya Arsenal na Liverpool. Grealish amekuwa akianzia benchi au kutokucheza na hii inachangia kutaka kuondoka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: