Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man City kumtumia Silva ili kumpata Joao Neves

Joao Neves Man City kumtumia Silva ili kumpata Joao Neves

Sun, 9 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Machester City inamtumia kiungo wao Bernando Silva Joao Neves, ili kumshawishi kiungo wa Benfica, Joao Neves akubali kujiunga nao katika dirisha hili.

Mabosi wa Man City wanatumia nguvu hiyo kutokana na upinzani mkubwa wanaoupata kutoka kwa Manchester United ambayo inahitaji huduma yake pia.

Joao mwenye umri wa miaka 19, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.

Benfica ipo tayari kumuuza kiungo huyu lakini ripoti zinaeleza inahitaji zaidi ya Euro 80 milioni ingawa kuingia kwa Man City kwenye dili hili pia huenda ikasababisha Benfica izidishe bei zaidi kutokana na uhitaji wa vigogo hawa.

Kiungo huyu wa kimataifa wa Ureno ambaye ni mmoja kati ya mastaa tegemeo wa Benfica msimu uliomalizika amecheza mechi 55 za michuano yote, amefunga mabao matatu na kutoa asisti mbili.

Man United inataka kuimarisha kikosi chake na imefungulia mastaa wengi mlango wa kutoka na itabidi ipambane kweli na City kuinasa huduma ya Nevez.

Caoimhin Kelleher

KIPA namba mbili wa Liverpool, Caoimhin Kelleher ambaye inadaiwa kuomba kuondoka katika dirisha hili, ameingia kwenye rada za Celtic na Brentford ambazo zipo tayari kutoa zaidi ya Pauni 15 milioni kwa ajili ya kumpata kipa huyu raia wa Ireland mwenye umri wa miaka 25. Kelleher ameomba kuondoka Liverpool kwa sababu anataka timu itakayompa nafasi yakuwa kipa namba moja na uwezekano wa hilo ni kwenye timu nyingine na siyo Anfield.

Alan Varela

Liverpool imeulizia uwezekano wa kumsajili kiungo wa FC Porto na Argentina Alan Varela, 22, katika dirisha hili. Benchi la ufundi ka Liverpool chini ya Kocha Arne Slot limevutiwa na ripoti ya maskauti iliyowasilishwa mezani kwao ikimwelezea kiungo huyu ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Katika msimu uliomalizika Varela amecheza mechi 44 za michuano yote na ameonyesha kiwango bora.

Chris Fuhrich

TOTTENHAM na Bayern Munich zimeingia vitani kuiwania saini ya winga wa Stuttgart, Chris Fuhrich katika dirisha hili. Winga huyu raia wa Ujerumani alionyesha kiwango bora msimu uliomalizika kiasi cha kuvutia vigogo wengi barani Ulaya wanaohitaji kuipata saini yake. Mkataba wa sasa wa Chris unamalizika mwaka 2028, msimu huu amecheza mechi 38 za michuano yote na kufunga mabao tisa.

Jake O’Brien

BORUSSIA Dortmund inafikiria kutuma wawakilishi wake Ufaransa kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Olympique Lyon kwa ajili ya kuipata saini ya beki wa timu hiyo na Ireland, Jake O’Brien, 23, katika dirisha hili. Staa huyu pia huduma yake inahitajika na Everton na AC Milan. Dortmund imevutiwa kutaka kumsajili staa huyu kutokana na kiwango bora alichoonyesha msimu uliomalizika.

Paolo Dybala

MANCHESTER United ni miongoni mwa timu zinazodaiwa kutaka kumsajili mshambuliaji wa AS Roma Paolo Dybala katika dirisha hili. Dyabala mwenyewe ameonyesha nia ya kutaka kuondoka Italia na kutua England na taarifa zinadai kuna uwezekano akauzwa kwa kiasi kisichozidi Pauni 10.2 milioni kwa mujibu wa kipengele kilichopo kwenye mkataba wake.

Staa huyu wa kimataifa wa Argentina msimu uliomalizika alifunga mabao 10 katika mechi 39 za michuano yote.

Xavi Simon

BAYERN Munich imeanza mazungumzo na Paris Saint-Germain kuipata saini ya kiungo wa timu hiyo, Xavi Simons, ambaye msimu uliomalizika alicheza kwa mkopo RB Leipzig. Xavi ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027, msimu uliomalizika alicheza mechi 43 za michuano yote, amefunga mabao 10 na kutoa asisti 15.

Lutsharel Geertruida

Liverpool imeshaanza mawasiliano na Feynoord kwa ajili ya kumsajili beki wa timu hiyo, Lutsharel Geertruida, 23, ambaye jina lake limependekezwa na kocha wao mpya, Arne Slot anayehitaji asajiliwe mara tu baada ya kuanza kazi kwenye timu hiyo. Staa huyu wa kimataifa wa Uholanzi huduma yake pia inahitajika na Tottenham, Newcastle na West Ham.

Chanzo: Mwanaspoti