Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man City kumpa Mkataba mpya Kevin De Bruyne

KDB DD Kiungo wa Man City, Kevin de Bruyne

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Manchester City ipo tayari kumsainisha mkataba mpya kiungo wake kutoka Ubelgiji, Kevin de Bruyne siku chache zijazo ili kumzuia asiondoke klabuni hapo.

Inadaiwa kuwa De Bruyne mwenyewe anahitaji kuendelea kusalia England kwa sababu ya familia yake imezoea zaidi maisha ya Jiji la Manchester.

Kiungo huyo ambaye msimu huu alianza vibaya kutokana na majeraha, kwa sasa amerejea na alionyeha kiwango bora kwenye mchezo dhidi ya Newcastle ambapo Man City ilishinda mbao 3-2.

De Bruyne ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2025, msimu huu amecheza mechi nne za michuano yote na amekuwa akiwindwa na vigogo wa Saudia tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi.

Awali, ripoti zilikuwa zinadai kuwa Man City ilikuwa tayari kumuachia ikiwa De Bruyne mwenyewe angeomba kuondoka. Huko Saudia timu kibao zimemuahidi mshahara mnono.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live