Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man City kumalizana na Akanji

Skysports Akanji Dortmund Man City 5881245 Manuel Akanji

Wed, 31 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Manchster City ya Uingereza inakaribia kumsajili mchezaji wa Borrusia Dortmund Manuel Akanji ambaye amekuwa akicheza kama beki wa kati huko Dortmund. City wana uhakika wa kuwasali wa Akanji klabuni hapo kabla ya dirisha hili kufungwa hapo kesho.

Manchester City ambao ndio mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza wameamua kufanya usajili katika eneo la ulinzi kwani kumekuwa na ushindani mkubwa sana katika ligi lakini vilevile kuimarisha eneo hili ili kutoruhusu mabao mengi msimu huu.

Akanji ataenda kuungana na mabeki wenzie kama kina Walker, Ruben Diaz, John Stones, Cancelo, Laporte, pamoja na Sergio Gomez kwa ajili ya kutetea ubingwa wao walioupata mara mbili mfufulizo.

Pep Guardiola akiwa kama kocha mkuu wa klabu hiyo amesajili mshambuliaji mfungaji Erling Braut Haaland kitu ambacho hakuwa nacho msimu uliopita lakini pia amemuuza Gabriel Jesus, Raheem Sterling ambao hawa wote walikuwa na mchango mkubwa kwenye timu yake . Vijana wa Pep kwenye mechi nne walizocheza wameshinda tatu na sare moja huku Erling Haaland akiwa ni mchezaji wa kwanza kupiga hattrick msimu huu pale Epl.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live