Ndege iliyowabeba wachezaji wa Manchester City wakati wanarejea England, ilipata hitilafu wakati ikiwa angani na kulazimika kutua katika jiji la Liverpool badala ya Manchester.
Tukio hilo limetokea wakirejea kutoka Ureno walikoshinda mabao 5-0 dhidi ya Sporting Lisbon
Chanzo cha hitilafu hiyo kwenye ndege hiyo aina ya Titan Airways Boeing 757, ni baada upepo mkali kuvuma na kusababisha ndege kuyumba na kutoa moshi, lakini rubani walilazimisha ndege hiyo kutua salama kwa dharura kwenye uwanja wa ndege wa Jonh Lennon jijini Liverpool.
Uongozi wa klabu wa Man City umetoa taarifa kuhusu tukio hilo kupitia akaunti yao ya Twitter, kwamba hitilafu ya ndege imetokea lakini wanashukuru wametua salama na hakuna aliyedhurika.
“Tunathibitisha kutokea kwa tukio hilo la kiufundi kwenye ndege yetu iliyobeba wachezaji wa kikosi cha kwanza, hiyo ni kutokana na upepo mkali kuvuma na kulazimisha ndege yetu kutua uwanja wa ndege wa Liverpool,”