Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man City, Liverpool zagongana kwa Musiala

Jamal Musiala Man City, Liverpool zagongana kwa Musiala

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: Dar24

Manchester City imeingia kwenye vita dhidi ya Liverpool kwenye mchakato wa kuiwania huduma ya kiungo wa Bayern Munich, Jamal Musiala kuelekea dirisha lijalo.

Musiala mwenye umri wa miaka 20, mkataba wake unamalizika mwaka 2026, hivi karibuni aliripotiwa kuwa kwenye rada za Liverpool inayomtaka ili kusuka upya eneo lake la kiungo linaloonekana kuwa na upungufu kwa msimu huu.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi tisa za michiano yote, amefunga bao moja na kutoa asisti mbili.

Kocha wa Man City anadaiwa kuzungumza na Musiala kwa njia ya simu akimshawishi ajiunge na kikosi chake ifikapo mwishoni mwa msimu huu.

Staa huyu alionyesha kiwango bora kwa msimu uliopita ambapo alifunga mabao 16 na kutoa asisti l6 kwenye mechi 47 za michuano yote alizocheza.

Hakuna taarifa kamili juu ya kiasi gani kitahitajika ili Bayern Munich kumwachia staa huyu ambaye pia inapambana kutaka kumsainisha mkataba mpya ili kumzuia asiondoke.

Chanzo: Dar24