Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man City, Liverpool kuivurugia Arsenal

Douglas Luiz Spec Douglas Luiz

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu za Manchester City na Liverpool zimeingilia kati dili la Arsenal kumwania nyota wa Aston Villa, kiungo Douglas Luiz.

Luiz mwenye umri wa miaka 25 alianza kuwindwa na Arsenal tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi na ilimhitaji ili akawe mbadala wa Thomas Partey anayehusishwa kutimkia Juventus dirisha lijalo.

Kutokana na ongezeko la timu zinazomhitaji, ripoti zinadai Aston Villa huenda ikapandisha bei ya kiungo huyu kufikia Pauni 50 miloni kutoka Pauni 25 milioni bei ya awali ambayo Arsenal ndio ilidaiwa inataka kuitoa.

Mkataba wa sasa wa kiungo huyu wa kimataifa wa Brazil unatarajiwa kumalizika mwaka 2026.

Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 20 za michuano yote, amefunga mabao sita na kutoa asisti matatu.

Man City wanamtaka Luiz akawe mbadala wa Kalvin Phillips huku Liverpool ikitaka kuimarisha safu yao ya kiungo na wawili hao wa nataka kuizidi kete Arsenal.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live