Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man City, Liverpool hakuna mbabe Etihad

IMG 6336.jpeg Mchezo ulimalizika kwa sare ya kufungana 1-1

Sun, 26 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi wa EPL, Manchester City wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Norway, Erling Haaland alianza kuifungia Manchester City dakika ya 27 akimalizia kazi nzuri ya beki Mholanzi, Nathan Benjamin Aké, kabla ya beki Muingereza, Trent John Alexander-Arnold kuisawazishia Liverpool dakika ya 80 akimalizia pigo la mshambuliaji Mmisri, Mohamed Salah.

Kwa matokeo hayo, Manchester City wanafikisha pointi 29 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi moja zaidi ya Liverpool inayofuatia nafasi ya pili baada ya wote kucheza mechi 13.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live