SUPERCOMPUTER imetabiri washindi wa Ligi ya Mabingwa msimu huu... na ni habari mbaya kwa mashabiki wa Chelsea.
Manchester City na Chelsea ndio wawakilishi wawili waliobaki Ligi Kuu England baada ya Liverpool na Tottenham kuambulia patupu katika hatua ya 16 bora.
Sasa Man City imepigiwa debe itanyakuwa ubingwa wa Ligi Mabingwa Ulaya mwaka huu katika fainali utakaochezwa jijini Instabul Juni 10 mwaka huu. Kwa mujibu wa 'Super Computer' Man City ina nafasi kubwa kufuatia ushindi mkubwa wa mabao 7-0 waliopata dhidi ya RB Leipzig.
Kwa upande mwingine Chelsea haikupewa nafasi ya kufika mbali kwenye michuano ya mwaka huu licha ya kutinga robo fainali kwa kishindo dhidi ya Borussia Dortmund baada ya kupindua matokeo.
Kikosi cha Graham Potter kimepewa asilimia 5 tu, AC Milan ikipewa asilimia chache mara mbili ya asilimia iliyopewa The Blues ambayo itacheza dhidi ya Read Madrid kwenye mechi robo fainali.
Hata kama Chelsea itafanikiwa kushinda dhidi ya Real Madrid, itamenyana na mshindi kati ya Bayern Munich na Man City katika mechi ya nusu fainali. Man City imepania kubeba ubingwa wa Ligi Mabingwa Ulaya wao wamepewa asilimia 28 na wana nafasi kubwa ya kunyakuwa ubingwa mwaka huu.
Hiyo ndiyo nafasi kubwa zilizopewa timu za kutoka England katika timu nane zilizofanikiwa kutinga robo fainali ya Ligi Mabingwa Ulaya.
Miamba ya Ujerumani ndio timu ya pili yenye uwezekano mkubwa wa kushinda shindano hilo, kwa mujibu wa 'Super Computer' hiyo yenye uwezo mkubwa, ikiwa na asilimia 18 ya nafasi.
Wachezaji wa Ligi ya Serie A, Napoli, ambao wanamenyana na AC Milan katika robo, wana nafasi ya tatu bora ya kushinda michuano hiyo.
Napoli hawajawahi kufika katika hatua ya nane bora ya Ligi ya Mabingwa, lakini sasa wana uwezekano kubeba ubingwa kwa asilimia 17. Mabingwa mara 14 wa michuano hii Real Madrid wamepewa asilimia 13, Benfica asilimia 10, Inter Milan asilimia sita.