Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamia ya wakazi wa Iringa wajitokeza kumzika Hans Pope

Zacharia Hans Poppe, Komandoo Marehemu Zacharia Hans Poppe enzi za uhai wake

Thu, 16 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamia ya wakazi wa mkoa wa Iringa na wadau wa soka wamejitokeza katika makaburi ya Makanyagio kumsindikiza katika safari yake ya mwisho aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope.

Marehemu Hans Poppe ambaye pia alikuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Simba, alifariki dunia Septemba 10, 2021 katika Hospitali ya Agha Kan, Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Akizungumza wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa la Jimbo la Iringa parokia ya Bikira Maria Consolata lililopo mshindo mjini hapo, Padri Idan Urungi alisema kifo ni ibada ambayo kila binadamu lazima aitumikie.

Amesema ni vizuri kumkumbuka Mungu wakati wa uhai ili kujiandaa vizuri kwa ajili ya safari ya mwisho.

Amesema marehemu Hans Poppe wakati wa uhai wake alikuwa mjasiri wa kuanzisha biashara na kutaka familia yake kuendeleza mshikamano.

“Tunamshukuru sana Hans Pope kwa ujenzi wa kanisa hili na ndio sababu ya familia kumleta marehemu kufanyiwa ibada ya mazishi hapa, kwani wanatambua mchango mkubwa aliokuwa akiutoa, tunashukuru pia kupata heshima hii ya kumfanyia ibada yake ya mwisho hapa," amesema.

Akizungumza mshauri wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya club hiyo, Crescentius Magori amesema kuwa marehemu Hans Pope alikuwa na mchango mkubwa katika soka la Tanzania kupitia klabu mbalimbali, ikiwemo Lipuli FC ya Iringa.

Nao mashabiki wa Simba mkoani hapo wamesema kuwa kifo cha Zakaria ni pigo kubwa kwa klabu ya Simba, hivyo watamuenzi kwa kufungua matawi mengi katika wilaya zote za Iringa.

Mungu ailaze roho ya Hans Pope mahali pema peponi, Amina.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live