Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamelodi yafumua kikosi chote kisa Yanga

Zxz Mamelodis Mamelodi Sundowns

Wed, 3 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Mamelodi Sundowns jana kilicheza mchezo wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL) na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Richards Bay, lakini kocha wa Masandawana, Rhulani Mokwena aliwapumzisha mastaa wake wote waliocheza dhidi ya Yanga.

Ushindi huo dhidi ya timu inayoshika nafasi ya pili kutoka mkiani, umeifanya Mamelodi kujiimarisha kileleni mwa msimamo kwa tofauti ya pointi 11 huku ikiwa na mechi mbili mkononi ikifukuzia ubingwa wa saba mfululizo wa PSL na wa 10 ndani ya misimu 12 tangu mwaka 2014.

Imefikisha pointi 49 kwenye mechi 19 ilizocheza, imeshinda mechi 15, sare nne na haijapoteza mchezo hata mmoja, ikiruhusu mabao matano tu. Imefunga mabao 34.

Kocha Mokwena kwenye mchezo wa jana alichezesha kikosi ambacho hakina nafasi kubwa ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza akianza na kipa mkongwe Dennis Onyango ambaye hajacheza muda mrefu kikosi cha kwanza.

Kama ilivyokuwa ilipoikabili Yanga, licha ya mabadiliko makubwa, Mamelodi ilicheza soka ililolizowea la kumiliki mpira kwa asilimia kubwa, nyota wake wakipiga mashuti 13 langoni kwa wapinzani na kufanikiwa kudumbukiza wavuni moja tu kati ya hayo.

Bao la ushindi kwenye mchezo huo lilifungwa baada ya dakika 90+ na Junior Mendieta.

Kwenye mchezo huo, Mamelodi walimiliki mpira kwa 79 asilimia huku wakiwaachia wapinzani wao asilimia 21 wakipiga mashuti manne tu langoni kwa wapinzani ambayo hayakuwa na madhara.

Wachezaji wengine walioanza kwenye mchezo huo ni Zuko Mdunyelwa, Terrence Mashego, Mothobi Mvala, Bathusi Aubaas, Sphelele Mkhulise, Lebohang Maboe, Sipho Mbule, Matias Esquivel, Tashreeq Matthews na Gaston Sirino.

Hicho ni kikosi tofauti na kilichocheza mechi ya awali ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga na kutoka 0-0 ugenini Kwa Mkapa, ambao walikuwa ni kipa Ronwen Williams, Khuliso Mudau, Divine Lunga, Mosa Lebusa, Gomolemo Kekane, Teboho Mokoena, Bongani Zungu, Marcelo Allende, Thembinkosi Lorch, Lucas Costa na Peter Shalulile.

Mamelodi itaikaribisha Yanga Ijumaa hii katika mechi yao ya marudiano ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika huko mjini Pretoria, ambako timu ya Wananchi inahitaji angalau sare ya mabao ili kuandika historia mpya kwa kutinga nusu fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live