Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamelodi yachungulia nusu fainali CAF

Mamelodi Sundowns SA Mamelodi yachungulia nusu fainali CAF

Mon, 24 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Timu mbili kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika zimepoteza michezo yao nyumbani, huku mechi za pili zikionekana kuwa za moto zaidi.

Michezo ya kwanza ya hatua hiyo ilifanyika juzi Jumamosi, ambapo katika Uwanja wa Mkapa Simba ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Wydad Casablanca.

Timu pekee ambayo imeanza kuchungulia nusu fainali ni Mamelodi Sundowns ambayo imefanikiwa kuwachapa CR Belouizdad mabao 4-1 nchini Algeria na sasa wanasubiri kwenda kumalizia kazi nyumbani kwao nchini Afrika Kusini.

Mamelodi ambao wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huu msimu huu, wamekuwa timu ya kwanza kushinda kwa mabao mengi katika hatua hii msimu huu, yakiwa yamefungwa na mastaa wake Peter Shililule ambaye alifunga mabao mawili na kufikisha matano kwenye chati ya ufungaji, lakini mengine yalifungwa na Cassius Mailula ambaye amefikisha manne na Noel Maema.

Mshindi wa jumla wa mechi hii atakutana na mshindi wa jumla kati ya Simba na Wydad ambapo mchezo wa kwanza Simba walishinda bao 1-0 kwenye Uwanja wa Mkapa, bao lililowekwa kimiani na Jean Baleke ambaye sasa amefikikisha mabao manne akiwa amelingana na Clatous Chama.

Mchezo mwingine uliwashuhudia mabingwa wa kihistoria wa michuano hii, Al Ahly wakiwa nyumbani kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kupunguza mzigo kwenye mchezo wa pili.

Ahly ambao wamekuwa bora kila wanapovuka hatua ya makundi walifunga mabao yao kupitia kwa Mohammed Abdelmonem na Hamdi Fathi, sasa wanatakiwa kupata sare au kupoteza kwa bao moja au kushinda mchezo wa ugenini Aprili 28 nchini Morocco.

Timu nyingine ambayo imepoteza nyumbani kwenye hatua hii ni JS Kabylie ambao walichapwa juzi na ES Tunis bao 1-0, hivyo wakiwa wamejiweka kwenye mlima mrefu wa kufuzu kwani watatakiwa kulazimika kupata ushindi nchini Tunisia Jumamosi, mshindi wa jumla hapa atakutana na mshindi wa mchezo wa Al Ahly na Raja.

Chanzo: Mwanaspoti