Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamelodi ya Wanawake wagawana bilioni 1 yote ya ubingwa

Mamelodi Sundowns Ladies Mamelodi Sundowns Ladies.

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamelodi Sundowns Ladies walipata Tsh billion 1 pesa ya Kitanzania baada ya kutwaa Ubingwa wa CAF Women's Champions League mwaka huu.

Pesa zote hizi waligawana wachezaji na benchi la ufundi ambao walikuwa pale Ivory Coast kwenye michuano hiii. Mabosi wa timu hii hawakuchukua hata sent Tano katika pesa hii iliyopatikana kwenye michuano hii ya Kinadada.

Kocha wa Mamelodi Sundowns Ladies Jerry Tshabalala amesema Mabosi wa Mamelodi Sundowns hawatafuti pesa katika Soka ila wameingia huku kusaka Mataji tuu hivyo hawana muda wa kung'ang'ania pesa ambayo imepambaniwa na wachezaji.

Utamaduni wa Mamelodi Sundowns wachezaji mkipambana ndani ya pitch mkatengeneza pesa nyingi katika michuano mtakayo shiriki hiyo ni pesa yenu yote gawaneni.

Kinachowafanya wachezaji wa Mamelodi Sundowns wajitume zaidi kwa timu zote mbili ni huu utamaduni wa wachezaji kugawana pesa zote zinazopatikana kwenye michuano yote wanayo shiriki.

Sasa kule mwituni unaweza kupigwa kombora ukiuliza pesa ya African Football League imeenda wapi #SundownsFC #Sundowns.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live