Mon, 25 Mar 2024
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Wapinzania wa Yanga SC kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Mamelodi Sundowns FC wamewatakia mashabiki wao wiki njema kwa kuandika kwa kutumia lugha ya Kiswahili.
Jambo hilo limetafsiriwa kama ni moja ya 'salamu' kwa wapinzani wao Yanga ambao wamekuwa na comments nyingi kwenye ukurasa wa Mamelodi Instagram wakitumia lugha ya Kiswahili.
Yanga anatarajia kupepetana na Mamelodi Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar ukiwa ni mchezo wa kwanza wa Robo Fainali kabla ya kurejeana huko Afrika Kusini Aprili 5, 2024.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live