Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamelodi watambe kwingine ila kwa Yanga wameyakanyaga - Kamwe

Mudathir Yahya Simuu Yanga vs Mamelodi ni Mudathir Day

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ali Kamwe ametangaza mechi yao ya robo fainali Klabu Bingwa Afrika Jumamosi hii dhidi ya Mamelodi Sundowns katika uwanja wa Mkapa, imepewa jina la” Muda Day”, maalumu kwa ajili ya mchezaji wao Mudathir Yahya.

Kamwe amesema hayo leo wakati akizindua kampeni za hamasa kwa mashabiki wa timu hiyo kuelekea mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya Masandawana kutoka kwa Madiba katika Dimba la Mkapa.

“Leo tunakwenda kuizindua hamasa kuelekea mechi yetu na Mamelodi, jina la mchezaji ambaye tumemkabidhi hii mechia maybe nyota zake zinasoma vizuri kwenda kumalizana na Masandawana.

“Baada ya kujadiliana na wachezaji, benchi la ufundi na viongozi tukaazimia kwa pamoja kwamba mechi hii apewe kijana mzawa kutoka Kizimkazi Zanzibar, Mudathir Yahya Abbas. Kwa hiyo mechi hii rasmi itakuwa ni Muda Day, simu ziite tukutane kwa Mkapa.

“Yani kazi ambayo tuko nayo sasa hivi ni kuwapigia simu wote waje kwa Mkapa, Watanzania wote watake wasitake watapokea simu zetu. Hata Mamelodi nimeona leo wameamka wamejiboost, na wao simu zetu zitaita kwao. Sisi kazi yetu ni kuhakikisha nchi inapata burudani.

“Jumamposi tunakwenda kumwambia Mamelodi kuna sehemu anazoweza kutamba lakini sio kwa Yanga na wala hataweza kututambia kwenye uwanja wetu, mbele ya watu wetu na ardhi yetu, tutatamba sisi wenyewe,” amesema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: