Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamelodi wapo 'siriazi' kumng'oa Aziz Ki, Motsepe aweka mkwanja

Stepahne Aziz KI Ahadi Aziz Ki

Mon, 20 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa zilizopo ni kwamba Mwenyekiti wa Mamelodi Sundowns, Tlhopie Motsepe amewasiliana na Agency inayomsimamia nyota wa Yanga SC, Stephan Aziz Ki inayojulikana kama Zambro Sport Management kuulizia upatikanaji wa kiungo huyo.

Mkataba wa Yanga SC na Stephan Aziz Ki unaelekea ukingoni na bado mazungumzo yanaendelea baina ya Yanga SC na wasimamizi wa raia huyo wa Burkina Faso juu ya kuongeza mkataba mpya.

Timu nyingine ambayo imeulizia upatikanaji wa Aziz Ki mbae amefunga magoli 15 kwenye NBC Premier League ni Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini huku Pyramid na Al Ahly wakitajwa kuwa kwenye mbio za kuwania saini ya kiungo huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live