Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamelodi wanafikirisha sana

Aziz Mokwena 2681708 Mamelodi wanafikirisha sana

Mon, 6 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamelodi Sundowns, binafsi wamenipa funzo kubwa sana pamoja na Mamlaka za soka Afrika Kusini, hii timu ilikuwa ina ratiba ngumu mnoo na michuano mingi mno ila wamepambana sana mpaka hapo nusu fainali.

Sundowns yupo Nusu fainali ya Nedbank Cup, anaongoza Ligi PSL, amebeba ubingwa wa African Football League na Nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa hapo bila kusahau michuano ya Telkom Knockout alishiriki, hakuna ratiba yoyote iliyobadilishwa as long as masaa 72 yalitimia Sundowns alicheza mechi.

Mfano alitoka kucheza robo fainali ya Nedbank akapumzika siku tatu akaenda kucheza Ligi Kuu kistha akasafiri kwenda Tunisia Champions League, akarudi akacheza Ligi kisha jana Champions League yani hakuna ratiba iliyosogezwa mbele ni mechi juu ya mechi hawa jamaa wamechoka sana, ratiba ngumu mno.

Binafsi naona wamepigana, kwao hawapati favor ya ligi yao kusimama week nzima kupisha maandalizi, imagine tarehe 20 April kacheza CAF, tarehe 23 Aprili kacheza Ligi halafu Tarehe 26 kacheza Champions League.

Huku kwetu tungeweza? Wamepigana sana wanakubwa na uchovu wa hali ya juu na ndio maana hata majeruhi ni wengi.

Halafu hapo hapo walikuwa na wacheza TISA kwenye kikosi cha Bafana Bafana pale AFCON tena wanaanza, wamecheza mechi nyingi sana na wakarudi wakacheza mechi za kirafiki za kalenda ya FIFA.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live