Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamelodi wamnyima Mayele visa kuingia Afrika Kusini

Mayele Sa Fiston Kalala Mayele.

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji kinara wa Klabu ya Pyramids FC, Fistoin Kalala Mayele amesema kuwa amenyimwa visa ya kuingia nchini Afrika Kusini wakati timu yake ilipokuwa ikisafiri kwa ajili ya mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mayele amethibitisha hilo baada ya mchezo huo kumalizika jana huku Pyramids wakifanikiwa kuwabana The Brazilian kwa kutoa nao sare ya bila kufungana Loftus Versfeld, Pretoria nchini Afrika Kusini, huku akiwakaribisha Misri ili awaonyeshe kazi.

"Sawa ulikataa kunipa visa ukiamini utatupiga, thubutu, point 1 muhimu, tukutane sasa Cairo."

Msimamo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Afrika umesimama hivi ambapo kila timu imeshinda mchezo mmoja, imepoteza mmoja na kutoa sare mchezo mmoja;

Msimamo

Sundowns (pointi 4)

TP Mazembe (4)

Nouadhibou (4)

Pyramids (4)



Shughuli ni pevu kundi A bado ni bichi, kuna tofauti ya alama sifuri kati ya kinara na mshika mkia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live