Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamelodi wamejichanganya tayari

Zxz Mamelodis Mamelodi wamejichanganya tayari

Tue, 26 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na mawasiliano wa Klabu ya Yanga, Ali Shabani Kamwe anasema kuwa anazo taarifa kutoka Afrika Kusini jinsi wanavyowazungumza Yanga SC.

Kamwe amesema hayo jana wakati akizindua hamasa kuelekea mchezo wa robo fainali ya CAFCL dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini utakaopigwa Jumamosi, Machi 30, 2024 katika Dimba la Mkapa majira ya saa 3:00 usiku.

“Juzi niligundua kuwa wengi wanaonunua tiketi za VIP wengi wanatoka nje ya nchi, kwa sababu tumepokea emails na simu nyingi kutoka Kenya, Uganda, Malawi na Zambia wakihitaji tiketi.

"Tumepata picha kwamba ukubwa wa hii mechi sio tu hapa Tanzania, hata mashabiki wa nchi za jirani wanataka kuishuhudia mechi yetu.

“Mechi yetu dhidi ya Mamelodi inazungumziwa Afrika nzima kwa sababu kwa sasa Mamelodi ndiyo timu yenye mvuto zaidi Afrika alafu Yanga ndiyo Suprise Package.

"Hata kwenye mijadala ya watu Afrika Kusini wanasema haupaswi kuichukulia poa Yanga kutokana na kile ilichokifanya msimu uliopita kwenye Kombe la Shirikisho kwa sababu wanaweza kukifanya kwenye Klabu Bingwa Afrika," amesema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: