Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamelodi wakijichanganya hapa tu, kwisha habari yao

Yanga Vs Mamelod 2nd Mamelodi wakijichanganya hapa tu, kwisha habari yao

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamelodi Sundowns 'Masandawana' wanatarajiwa kushuka dimbani leo kwenye mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Young AfricansSC 'Yanga'(PSL) pale dimba la Loftus Versfeld.

Katika mchezo huo wa marudiano, iwapo itatokea Mamelodi hawajapata goli ndani ya dakika 20 za kipindi cha kwanza za basi mechi itakuwa ngumu kwao.

Kwa nini itakuwa ngumu kwao? Kwa sababu ni kwamba Yanga watakuwa wameshawazoea Mamelodi.

Yanga ni wazuri zaidi kipindi cha pili, wakimsoma mpinzani kipindi cha kwanza na kutumia madhaifu yake kumwadhibu kipindi cha pili.

Takribani asilimia 80 ya magoli yao msimu huu, Yanga wamefunga katika kipindi cha pili. Rejea mechi ya Yanga 5-1, mechi ya CR Belouizdad bao 4-0 na hata mechi nyingine nyingintu za Ligi, kipindi cha pili Yanga wanakuwa na energy si ya kawaida ambapo timu nyingi hushindwa kuendana na mziki wao.

Kumbuka kuwa, sare kuanzia goli 1-1 itakuwa faida kwa Yanga kutinga nusu fainali ya CAFCL.

Tusubiri kuona maajabu ya soka kwenye ardhi ya Mzee Nelson Mandela Madiba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live